Sheka, ambaye kawaida yake hapendi kutumia pesa ovyo,  anaamua kujipenda kwa kununua simu mpya. Sheka anadhani amepata bonge la dili, kumbe kaingizwa mjini. Hebu chungulia Mapanki S01E10.

Hebu kongoli "Read More"...Mandela anaitwa kwenye usahili wa kazi. Kwa kuwa nafasi ya kazi alitafutiwa na rafiki yake, anakuwa na matumaini kwamba kazi angepata tu bila "motisha", kinyume chake anaondoka akiwa na hasira. Hebu chungulia Mapanki S01E08

Hebu kongoli Read More kupata uhondo...


Kwa sababu ya wivu ya mapenzi, Swagga anaamua kumfuatilia mpenzi wake ambaye amesikia yuko sehemu ya starehe na mwanaume mwingine. Matunda ya safari ya Swagga ni manundu usoni. Hebu chungulia Mapanki S01E07.

Hebu kongoli Read More kupata uhondo...Liko anajiunga na mpango wa kampuni moja ambayo anadhani ni ya Kimarekani ili apate faida ya haraka haraka. Kwa mshangao wake, anaingizwa mjini na kubaki na machungu. Hebu chungulia Mapanki S01E06.

Hebu kongoli Read More kupata uhondo

 Hatimaye....episode 5 ipo hapa. Hebu pata uhondo...
S1, Ep5
3rd Oct. 2015 Jana Kilinuka..!!
Swagga anapenda kupepesa macho kulia na kushoto. Tabia ya kupenda warembo mji mzima inamtokea puani pale zali linapotokea baada ya wapenzi wake wawili kugongana. Hebu chungulia Mapanki S01E05.
                                 


Tarehe rasmi ya kuruka S01Ep5 ilikuwa ni tarehe 13 June 2015, unaweza kutembelea link hizi ili kuangalia Episode zilizopita

Hatimaye....episode 4 imewadia. Hebu bonyeza "Read More" kupata uhondo...
S1, Ep4
26th Sept. 2015 Swagga, Lipa Deni..!
Swagga anakutana na kichapo toka kwa machinga muuza nguo baada kwa kushindwa kulipa deni la nguo. Baada ya kupata kichapo, vinyozi wenzake wanamuweka kati kumpa nasaha juu ya kupenda starehe na maisha yaliyo juu ya uwezo wake. Hebu chungulia Mapanki S01E04.
                                                                             


Tarehe rasmi ya kuruka S01Ep4 ilikuwa ni tarehe 06 June 2015, kwa unaweza kutembelea link hizi ili kuangalia Episode zilizopita