Mapanki S01E10 - Sheka, Aaah Hata na Wewe Unalizwa?

Sheka, ambaye kawaida yake hapendi kutumia pesa ovyo,  anaamua kujipenda kwa kununua simu mpya. Sheka anadhani amepata bonge la dili, kumbe kaingizwa mjini. Hebu chungulia Mapanki S01E10.

Hebu kongoli "Read More"...0 comments:

Chapisha Maoni

Mapanki S01E09 - Liko, Mjini Wajanja Wengi!

0 comments:

Chapisha Maoni

Episode 8: Mandela, Bila Motisha Bongo Haiendi...!

Mandela anaitwa kwenye usahili wa kazi. Kwa kuwa nafasi ya kazi alitafutiwa na rafiki yake, anakuwa na matumaini kwamba kazi angepata tu bila "motisha", kinyume chake anaondoka akiwa na hasira. Hebu chungulia Mapanki S01E08

Hebu kongoli Read More kupata uhondo...


0 comments:

Chapisha Maoni

Episode 7 - Swagga, Watakuua Bure!

Kwa sababu ya wivu ya mapenzi, Swagga anaamua kumfuatilia mpenzi wake ambaye amesikia yuko sehemu ya starehe na mwanaume mwingine. Matunda ya safari ya Swagga ni manundu usoni. Hebu chungulia Mapanki S01E07.

Hebu kongoli Read More kupata uhondo...0 comments:

Chapisha Maoni

Mapanki S01E06 - Liko, Kila King'aacho Si Dhahabu

Liko anajiunga na mpango wa kampuni moja ambayo anadhani ni ya Kimarekani ili apate faida ya haraka haraka. Kwa mshangao wake, anaingizwa mjini na kubaki na machungu. Hebu chungulia Mapanki S01E06.

Hebu kongoli Read More kupata uhondo

0 comments:

Chapisha Maoni

Episode 5: Jana Kilinuka..!!

 Hatimaye....episode 5 ipo hapa. Hebu pata uhondo...
S1, Ep5
3rd Oct. 2015 Jana Kilinuka..!!
Swagga anapenda kupepesa macho kulia na kushoto. Tabia ya kupenda warembo mji mzima inamtokea puani pale zali linapotokea baada ya wapenzi wake wawili kugongana. Hebu chungulia Mapanki S01E05.
                                 


Tarehe rasmi ya kuruka S01Ep5 ilikuwa ni tarehe 13 June 2015, unaweza kutembelea link hizi ili kuangalia Episode zilizopita0 comments:

Chapisha Maoni

Episode 4: Swagga Lipa Deni!Hatimaye....episode 4 imewadia. Hebu bonyeza "Read More" kupata uhondo...
S1, Ep4
26th Sept. 2015 Swagga, Lipa Deni..!
Swagga anakutana na kichapo toka kwa machinga muuza nguo baada kwa kushindwa kulipa deni la nguo. Baada ya kupata kichapo, vinyozi wenzake wanamuweka kati kumpa nasaha juu ya kupenda starehe na maisha yaliyo juu ya uwezo wake. Hebu chungulia Mapanki S01E04.
                                                                             


Tarehe rasmi ya kuruka S01Ep4 ilikuwa ni tarehe 06 June 2015, kwa unaweza kutembelea link hizi ili kuangalia Episode zilizopita


0 comments:

Chapisha Maoni

15 March 2015 Behind The Scene (MTAANI)

Ni siku Nyingine Tena, Hizi ni Picha Za Matukio yaliyojiri siku ya Tarehe 15 Marchi 2015 katika ukusanyaji wa Matukio nyuma ya Pazia. Pia kwa Bahati nzuri Mapanki ilipata Heshima ya kujitambulisha kwa Diwani wa Kata ya Rau iliyopo Moshi. Mh.Kitoto. aliyekuwepo eneo hilo ili kushuhudia namna kazi inavyoendelea, ndipo Baada ya Utambulisho kutoka Kwa Director Msaidizi ndugu Ditram Ngonyani, Mh.Kitoto aliweza kuitembelea Tovuti ya Mapanki na kuonesha kufurahishwa na Mradi mzima namna unavyowapa Vijana Shughuri za Kufanya.

Director Msaidizi ndugu Ditram Ngonyani, Aliyevalia shati la Draft akiitambulisha Mapanki kwa Diwani wa kata ya Rau iliyopo Moshi, MhKitoto

Director Msaidizi ndugu Ditram Ngonyani akimtambulisha Director Kiongozi Ndugu Fredy Okuku kwa Diwani, Mh Kitoto

Hapa Diwani akionesha kuifuatilia Mapanki Mtandaoni kupitia simu yake aliyoishika

Maigizo yakiendelea kwa Hakika Wenyeji wa kijiwe walionesha Ushirikiano Mkubwa sana kwa scene hii

Ditram Ngonyani
Director Msaidizi

0 comments:

Chapisha Maoni

MAPANKI NDANI YA BBC

Crew nzima ya MAPANKI iliweza kufanyiwa mahojiano na Shirika la Habari la BBC siku ya Tarehe 14 Marchi 2015, katika Ofisi za Habari Media Concertancy (HMC) zilizopo Moshi,
Jumamosi ya Jana ya tarehe 14 March 2015, imekuwa ni siku njema na Baraka katika ofisi za Habari media concertancy (HMC) zilizopo Moshi, hapa tulifanikiwa kuongea na Manager ambaye ndiye mwakilishi Wa Startv Moshi kuhusu Tamthilia ya Mapanki alionesha kuvutiwa na kulipenda sana wazo la Mapanki na kututia moyo sana, na kisha kupata kuhojiwa kuhusu Mapanki siku hiyo hiyo na Leonard Mubali mwanahabari wa shirika la habari la BBC.
Haya ni Matukio katika PichaHapa Wahusika wakuu Wa Tamthilia ya Mapanki Sheka na Mandela wakitoa igizo fupi katika kipaza sauti cha BBC

Hapa nikihojiwa kuhusu Tamthilia ya Mapanki na Mtangazaji Wa BBC ndugu Leonard Mubali Mahojiano na BBC yakiendeleaHapa Kwa niaba ya Mapanki Dir.Fredy Okuku alikuwa anaunda urafiki na Manager Wa Habari Media Concertancy (HMC) ambaye ndiye mwakilishi Wa Startv mkoani MoshiTukipata picha ya ukumbusho

Hatimaye Director Fredy Okuku akitoa shukrani zake kwa Shirika la Habari la BBC kwa mchango wao kwa Vijana

0 comments:

Chapisha Maoni