Kutana na Hassan Mashaka - "Liko"

Hassan amezaliwa kama miaka 28 iliyopita na alianza kuipenda sanaa tokea alipokuwa darasa la 7. Marafiki zake wengi walimwambia ana kipaji mpaka wakampa jina la utani la "Msanii". Kwa sababu ya motisha aliyopewa, alijituma na kuendelea kujifunza mambo mengi ya sanaa.
Katika tasnia ya filamu, Hassan amewahi kucheza filamu ya NIFUNDISHE KUPENDA akiwa katika kundi la Mng'ao Sanaa Group.
Anaipenda MAPANKI kwa sababu inazungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
"Watanzania wakae mkao wa kula. Tumekuja kufanya mapinduzi katika tasnia ya filamu Tanzania", anasema Hassan.

0 comments:

Chapisha Maoni

Nyuma ya Pazia

Mambo lazima yawekwe mguu sawa...au siyo?


Tukutane February 7, 2015 episode ya kwanza itakaporuka hewani...


0 comments:

Chapisha Maoni

SWAGA-licious

SWAGA-licious...nyuma ya pazia, vijana wakipanga mikakati...

Tukutane February 7, 2015 episode ya kwanza itakaporuka hewani...


0 comments:

Chapisha Maoni

Kutana na Ditram Pacominus Ngonyani - " Sheka"

Amezaliwa miaka 30 iliyopita katika Mkoa wa Ruvuma na ana elimu ya kidato cha nne. Kwa upande wa sanaa, Ditram yuko katika ngazi za awali.

Ditram alianza sanaa mwaka 2008 na mpaka sasa amecheza filamu moja ya NIFUNDISHE ambayo iliongozwa na director wa MAPANKI, Fredy Okuku.

Kwenye tamthilia hii ya MAPANKI amecheza kama Sheka, kijana ambaye ni bahili sana. "Matarajio yangu ni kwamba MAPANKI itakuwa sehemu ya kutimiza ndoto zangu kwa jinsi ambavyo script imeandikwa pamoja na director ambaye ameongoza" anasema Ditram.

Anaamini pia MAPANKI itabadilisha fikra za wengi.


0 comments:

Chapisha Maoni

Kutana na Aziz Salim Mpai - "Swaga"

Amezaliwa miaka kama 22 iliyopita na safari yake ya sanaa ilianza rasmi April 2010 katika kikundi cha sanaa cha Red Apple kilichopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro. Alijiunga na kikundi cha Red Apple baada ya kushawishiwa na watu wengi, wakiwemo wazazi wake, baada ya kuona kipaji chake. MAPANKI ndiyo kazi yake rasmi ya kwanza. Tamthilia hii imemvutia kutokana na ufundi mkubwa uliotumika kuandaa kazi, kuanzia muswada/script mpaka utayarishaji rasmi. "Nimefurahi kuicheza nafasi ya Swaga kwa sababu imenifanya nijifunze mambo mengi sana katika sanaa" anasema Aziz. Malengo ya Aziz ni kufanya makubwa katika tasnia ya filamu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha mfumo mzima. Anawashukuru wote waliomfanikisha kushiriki katika tamthilia hii, akiwemo director, aliyemsaidia kujifunza mengi.

0 comments:

Chapisha Maoni

MAPANKI PROMO episode 1

At last the promo is here. Welcome to Watch while waiting for the full 10 min show on 7the February 2015, Atimaye video fupi ya tangazo ipo hapa. Karibu kuitazama wakati ikisubiri burudani nzima ya Dk 10 siku ya tare he 7 februari 20150 comments:

Chapisha Maoni

Episode One Snapshot

Hizi ni Picha halisi zilizokamatwa katika Tamthilia ya Mapanki Sehemu ya Kwanza, Zinaonesha Ubora uliotumika na Rangi inaopendezesha Macho, kaa Tayari kwa Kifaa hiki kinachokuja Tarehe 7 Frebruari 2015

1 comments:

Chapisha Maoni

COMING SOON

Hatimaye tamthilia iliyokuwa katika mikakati ya kuleta mapinduzi inayokuja kwa jina la MAPANKI, imeanza kufanyiwa kazi katika Studio ya STARSHA FILM STUDIO yenye ofisi Mkoani Dodoma Tanzania. Hii ni tamthilia ya mtandaoni itakayorushwa hewani katika mtandao huu kwa mfululizo.

Baada ya kusafiri mpaka Moshi na kukuta vipaji vya vijana wasiovuma kisanaa, lakini wenye shahuku ya kuwa mastar, Director Fredy Okuku aliweza kufanya nao kazi kuanzia tarehe 3 Januari 2015 mpaka tarehe 7 Januari 2015. Vijana walionesha ushirikiano mkubwa sana.

Tarehe rasmi ya Sehemu ya Kwanza ya tamthilia kurushwa mtandaoni ni tarehe 7th Februari 2015.

Jina: MAPANKI
Wahusika wakuu: Ditram Ngonyani, Cosmas Peter, Hassan Mashaka, Aziz Salim
Mtunzi: Metty Nyang'oro
Director: Fredy S. Okuku
Studio: STARSHA FILM STUDIO
Tarehe ya kutolewa Sehemu ya kwanza; 7 Februari 2015
 

0 comments:

Chapisha Maoni