COMING SOON

Hatimaye tamthilia iliyokuwa katika mikakati ya kuleta mapinduzi inayokuja kwa jina la MAPANKI, imeanza kufanyiwa kazi katika Studio ya STARSHA FILM STUDIO yenye ofisi Mkoani Dodoma Tanzania. Hii ni tamthilia ya mtandaoni itakayorushwa hewani katika mtandao huu kwa mfululizo.

Baada ya kusafiri mpaka Moshi na kukuta vipaji vya vijana wasiovuma kisanaa, lakini wenye shahuku ya kuwa mastar, Director Fredy Okuku aliweza kufanya nao kazi kuanzia tarehe 3 Januari 2015 mpaka tarehe 7 Januari 2015. Vijana walionesha ushirikiano mkubwa sana.

Tarehe rasmi ya Sehemu ya Kwanza ya tamthilia kurushwa mtandaoni ni tarehe 7th Februari 2015.

Jina: MAPANKI
Wahusika wakuu: Ditram Ngonyani, Cosmas Peter, Hassan Mashaka, Aziz Salim
Mtunzi: Metty Nyang'oro
Director: Fredy S. Okuku
Studio: STARSHA FILM STUDIO
Tarehe ya kutolewa Sehemu ya kwanza; 7 Februari 2015
 

0 comments:

Chapisha Maoni