Kutana na Aziz Salim Mpai - "Swaga"

Amezaliwa miaka kama 22 iliyopita na safari yake ya sanaa ilianza rasmi April 2010 katika kikundi cha sanaa cha Red Apple kilichopo Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro. Alijiunga na kikundi cha Red Apple baada ya kushawishiwa na watu wengi, wakiwemo wazazi wake, baada ya kuona kipaji chake. MAPANKI ndiyo kazi yake rasmi ya kwanza. Tamthilia hii imemvutia kutokana na ufundi mkubwa uliotumika kuandaa kazi, kuanzia muswada/script mpaka utayarishaji rasmi. "Nimefurahi kuicheza nafasi ya Swaga kwa sababu imenifanya nijifunze mambo mengi sana katika sanaa" anasema Aziz. Malengo ya Aziz ni kufanya makubwa katika tasnia ya filamu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha mfumo mzima. Anawashukuru wote waliomfanikisha kushiriki katika tamthilia hii, akiwemo director, aliyemsaidia kujifunza mengi.

0 comments:

Chapisha Maoni