Kutana na Ditram Pacominus Ngonyani - " Sheka"

Amezaliwa miaka 30 iliyopita katika Mkoa wa Ruvuma na ana elimu ya kidato cha nne. Kwa upande wa sanaa, Ditram yuko katika ngazi za awali.

Ditram alianza sanaa mwaka 2008 na mpaka sasa amecheza filamu moja ya NIFUNDISHE ambayo iliongozwa na director wa MAPANKI, Fredy Okuku.

Kwenye tamthilia hii ya MAPANKI amecheza kama Sheka, kijana ambaye ni bahili sana. "Matarajio yangu ni kwamba MAPANKI itakuwa sehemu ya kutimiza ndoto zangu kwa jinsi ambavyo script imeandikwa pamoja na director ambaye ameongoza" anasema Ditram.

Anaamini pia MAPANKI itabadilisha fikra za wengi.


0 comments:

Chapisha Maoni