Kutana na Hassan Mashaka - "Liko"

Hassan amezaliwa kama miaka 28 iliyopita na alianza kuipenda sanaa tokea alipokuwa darasa la 7. Marafiki zake wengi walimwambia ana kipaji mpaka wakampa jina la utani la "Msanii". Kwa sababu ya motisha aliyopewa, alijituma na kuendelea kujifunza mambo mengi ya sanaa.
Katika tasnia ya filamu, Hassan amewahi kucheza filamu ya NIFUNDISHE KUPENDA akiwa katika kundi la Mng'ao Sanaa Group.
Anaipenda MAPANKI kwa sababu inazungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
"Watanzania wakae mkao wa kula. Tumekuja kufanya mapinduzi katika tasnia ya filamu Tanzania", anasema Hassan.

0 comments:

Chapisha Maoni