Hatuko Hewani Wiki Hii



Kutokana na sababu zilizo nje wa uwezo wetu, Mapanki haitokuwa hewani wiki hii. Lakini tunaendelea na upishi, na tunawahakikishia kwamba yanayokuja ni matamu zaidi...

Wakati tukisubiri, hebu burudika na hii filamu fupi iliyotayarishwa na director wa Mapanki, Fredy Okuku:





0 comments:

Chapisha Maoni

Mapanki - Episode 3 - Mandela na Mtendaji




Mandela anakutana na joto la Ofisi ya Mtendaji kwa kunyimwa huduma mpaka atoe chochote ili ahudumiwe. Kwa hasira Mandela anawasili saluni na kuyageuza maongezi ya vinyozi wenzake, huku wote wakionesha maumivu yao juu ya nchi na viongozi wake.

Je, nini kilitoka mioyoni mwao? Ebu chungulia Mapanki S01E03





0 comments:

Chapisha Maoni

Episode Three Snapshot

Hizi ni Picha halisi zilizokamatwa katika Tamthilia ya Mapanki Sehemu ya Tatu, Zinaonesha Ubora uliotumika na Rangi inaopendezesha Macho, kaa Tayari kwa Sehemu  ya tatu Tarehe 21 February 2015.














0 comments:

Chapisha Maoni

Mapanki - Episode 2 - Ubahili wa Sheka


Baada ya binti yake kuonesha dalili za ugonjwa, Sheka anatafuta namna ya kukwepa kumpeleka hospitali ili kuzuia fedha kutumika huku akilalamikiwa na mke wake. Anapolalamika kuhusu mke wake kuwa na matatizo, vinyozi wenzake wanamweka Sheka kitimoto na kumuonesha kwamba tatizo ni ubahili wake.
Ebu chungulia Mapanki S01E02.







0 comments:

Chapisha Maoni

Episode TWO Snapshot

Hizi ni Picha halisi zilizokamatwa katika Tamthilia ya Mapanki Sehemu ya Pili, Zinaonesha Ubora uliotumika na Rangi inaopendezesha Macho, kaa Tayari kwa Sehemu  ya pili Tarehe 14 February 2015.












0 comments:

Chapisha Maoni

Tumetua: Season 1, Episode 1


 Swagga za Swagga
Baada ya mtindo wake wa maisha kuwa juu kinyume na kipato chake, Swaga anabanwa na maswali mazito kutoka kwa vinyozi wenzake na kufanya siri kubwa kufichuka. Je, ni siri gani hiyo?, Ebu chungulia Mapanki S01E01.





0 comments:

Chapisha Maoni

Tunakuja February 7, 2015

Tunakuja February 7, 2015.
Ukiiona tamthilia ya Mapanki kwa mara ya kwanza, usishangae kwa nini tamthilia yetu  i
na urefu wa kama dakika 10 tu hivi.
Kwa nini tumeamua tamthilia ya Mapanki iwe na urefu wa dakika 10 badala ya dakika 30 mpaka 60? Ni kwa sasabu mpango wetu ni kuonesha tamthilia yetu kupitia mtandao tu. Kwa kawaida, vitua vya luninga vinahitaji vipindi vya tamthilia viwe na urefu wa dakika 30 mpaka 60. Sisi lengo letu ni kukupa burudani bila kubanwa na fomula za vituo vya luninga.
Ndo ubunifu wenyewe huo, au siyo?

0 comments:

Chapisha Maoni

Kutana na Cosmas Peter - "Mandela"

Cosmas amezaliwa Babati miaka 24 iliyopita. Sanaa ameanza toka yuko shule ya msingi, ambako alikuwa anatunga maigizo na kuigiza.

Alipomaliza shule akajiunga na kikundi cha Sanaa Mng'ao. Katika tasnia ya filamu, Cosmas ameshiriki katika filamu ya NIFUNDISHE KUPENDA ambayo bado ipo katika maandalizi.

"Mapanki kwangu ni tamthilia bora ambayo imeandaliwa kwa hadhi ya kimataifa kuanzia muongozo hadi uandaaji", anasema Cosmas.

Ndoto za Cosmas ni kuwa msanii wa kimataifa. Pia atanamani kutumia kipaji chake kuwaelimisha vijana wenzake. Hali kadhalika, anatamani kusoma sanaa kwenye vyuo vikubwa kama Cambridge University au Hollywood Art School.

0 comments:

Chapisha Maoni