Kutana na Cosmas Peter - "Mandela"

Cosmas amezaliwa Babati miaka 24 iliyopita. Sanaa ameanza toka yuko shule ya msingi, ambako alikuwa anatunga maigizo na kuigiza.

Alipomaliza shule akajiunga na kikundi cha Sanaa Mng'ao. Katika tasnia ya filamu, Cosmas ameshiriki katika filamu ya NIFUNDISHE KUPENDA ambayo bado ipo katika maandalizi.

"Mapanki kwangu ni tamthilia bora ambayo imeandaliwa kwa hadhi ya kimataifa kuanzia muongozo hadi uandaaji", anasema Cosmas.

Ndoto za Cosmas ni kuwa msanii wa kimataifa. Pia atanamani kutumia kipaji chake kuwaelimisha vijana wenzake. Hali kadhalika, anatamani kusoma sanaa kwenye vyuo vikubwa kama Cambridge University au Hollywood Art School.

0 comments:

Chapisha Maoni