MRADI/ THE PROJECT

MAPANKI: Kwa Mtandao, Kwa Watanzania


Matumizi ya mtandao ndani ya Afrika, na hususan Tanzania, yanaongezeka. Ni jambo lisilo na ubishi kwamba mtandao umeleta mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali kama vile benki, elimu, na vyombo vya habari. Mtandao umeleta mapinduzi makubwa kwenye mfumo ambao watumiaji wa vyombo habari wanavyopashwa habari. Mtandao umewawezesha watumiaji wa habari kupata habari kwa jinsi wanavyotaka wao – mahali popote na wakati wowote.

Kwa kutambua haya mabadiliko makubwa yanayotokea katika tasnia ya habari, makampuni mawili – Sendoland Media na Starsha Film Studio, yameingia katika mkakati wa kuleta tamthilia ya MAPANKI ambayo itaoneshwa mtandaoni tu.  Siyo tu kwamba Sendoland Media na Starsha Film Studio inaleta changamoto kwenye njia ya ugavi wa filamu na tamthilia, kampuni hizi zimeamua kuachana na mfumo wa kutengeneza tamthilia ya kwa dakika 30 mpaka 60, badala yake MAPANKI itakuwa ni tamthilia ya urefu wa dakika 10 tu!

Kwa hiyo kaa mkao wa kula upate uhondo
__________________________

MAPANKI: Online, For Tanzanians


Internet access across Africa, and Tanzania in particular, is growing. It is undeniable that internet access has had a major positive impact on many areas such as banking, education, and media. The internet has revolutionized the means by which media consumers get access to content. Internet access has enabled media consumers to have access to information on their terms – anywhere and anytime.  

In recognition of the changes in the media landscape, two media companies - Sendoland Media and Starsha Film Studio, are on a mission to bring MAPANKI as an online only drama series. Sendoland Media and Starsha Film Studio are not only challenging the film and drama distribution method by bypassing the traditional television sets, we also ignoring the traditional 30 to 60 minutes format, as MAPANKI drama series will only be 10 minutes long!

So just sit back and enjoy. 

0 comments:

Chapisha Maoni