TAZAMA ONESHO / WATCH THE SERIES

Season 1

_________________________________________________________________________________

S1, Ep1
7th Feb. 2015 Swagga za Swagga
Baada ya mtindo wake wa maisha kuwa juu kinyume na kipato chake, Swaga anabanwa na maswali mazito kutoka kwa vinyozi wenzake na kufanya siri kubwa kufichuka. Je, ni siri gani hiyo?, Ebu chungulia Mapanki S01E01.
_________________________________________________________________________________

S1, Ep2
14th Feb. 2015 Sheka, acha ubahili..!!
Baada ya Binti yake kuonesha dariri za ugonjwa, Sheka anatafuta namna ya kukwepa kumpeleka Hospitali ili kuzuhia fedha kutumika huku akilalamikiwa na Mke wake kisha kuwekwa kitimoto na Vinyozi wenzake. Je, nini kiliendelea?, Ebu chungulia Mapanki S01E02.
                          Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep3
21th Feb. 2015 Mandela, unakuwa kama vile Bongo uhijui..!!
Mandela anakutana na Joto la Ofisi ya Mtendani kwa kunyimwa huduma Baada ya kutokubaliana na Mtendaji katika suala la kumpa chochote ili ahudumiwe. Ndipo kwa hasira Mandela anawasili Saluni na kuyageuza maongezi ya Vinyozi wenzake, huku wote wakionesha Maumivu yao juu ya Nchi na Viongozi wake. Je, nini kilitoka mioyoni mwao?, Ebu chungulia Mapanki S01E03.
                                                                              Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep4
26th Sept. 2015 Swagga, Lipa Deni..!
Swagga anakutana na kichapo toka kwa machinga muuza nguo baada kwa kushindwa kulipa deni la nguo. Baada ya kupata kichapo, vinyozi wenzake wanamuweka kati kumpa nasaha juu ya kupenda starehe na maisha yaliyo juu ya uwezo wake. Hebu chungulia Mapanki S01E04.
                                                                              Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep5
3rd Oct. 2015 Jana Kilinuka..!!
Swagga anapenda kupepesa macho kulia na kushoto. Tabia ya kupenda warembo mji mzima inamtokea puani pale zali linapotokea baada ya wapenzi wake wawili kugongana. Hebu chungulia Mapanki S01E05.
                                  Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep6
10th Oct. 2015 Liko, Kila King'aacho Si Dhahabu
Liko anajiunga na mpango wa kampuni moja ambayo anadhani ni ya Kimarekani ili apate faida ya haraka haraka. Kwa mshangao wake, anaingizwa mjini na kubaki na machungu. Hebu chungulia Mapanki S01E06.
                                  Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep7
17th Oct. 2015 Swagga, Watakuua Bure...
Kwa sababu ya wivu ya mapenzi, Swagga anaamua kumfuatilia mpenzi wake ambaye amesikia yuko sehemu ya starehe na mwanaume mwingine. Matunda ya safari ya Swagga ni manundu usoni. Hebu chungulia Mapanki S01E07.
                                  Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep8
24th Oct. 2015 Mandela, Bila Motisha Bongo Haiendi...!
Mandela anaitwa kwenye usahili wa kazi. Kwa kuwa nafasi ya kazi alitafutiwa na rafiki yake, anakuwa na matumaini kwamba kazi angepata tu bila "motisha", kinyume chake anaondoka akiwa na hasira. Hebu chungulia Mapanki S01E08.
                                  Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep9
31st Oct. 2015 Liko, Mjini Wajanja Wengi!
Liko anapopewa mchongo wa kupeleka mahindi Zambia, anaamua kuichangamkia nafasi. Alichokosea kijua ni kwamba mjini wajanja wengi. Hebu chungulia Mapanki S01E09.
                                  Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

S1, Ep10
7th Nov. 2015 Sheka, Aaah Hata na Wewe Unalizwa?
Sheka, ambaye kawaida yake hapendi kutumia pesa ovyo,  anaamua kujipenda kwa kununua simu mpya. Sheka anadhani amepata bonge la dili, kumbe kaingizwa mjini. Hebu chungulia Mapanki S01E10.
                                  Tazama Onesho Zima
_________________________________________________________________________________

0 comments:

Chapisha Maoni